June 15, 2021


KWENYE mchezo wa Copa America uliochezwa usiku wa kuamkia leo Juni 15, timu ya taifa ya Argentina imetoshana nguvu na Chile kwa kufungana bao 1-1.

Lionel Messi alipachika bao bora kwa pigo huru dakika ya 33 liliwekwa usawa na Eduardo Vargas dakika ya 57.

Licha ya Messi kupachika bao hilo bora akiwa umbali wa yard 25 waliweza kuacha pointi mbili katika mchezo huo ambao ulikuwa na ushindani mkubwa uliochezwa Uwanja wa Olympic.

Kwenye mchezo huo Argertina walipiga jumla ya mashuti 18 na matano yalilenga lango huku Chile wakifanya hivyo mara 5, katika mashuti hayo ni manne yalilenga lango.

Kwenye msimamo wa kundi B, Paraguay inaongoza kundi ikiwa na pointi tatu huku Argertina na Chile zikiwa na pointi moja na Uruguay haina pointi sawa na Bolivia.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic