UONGOZI wa Simba umeweka wazi kwamba upo tayari kwa ajili ya mechi zao ambazo zimebaki ndani ya ligi ikiwa ni pamoja na ule dhidi ya Polisi Tanzania.
Mchezo wao ujao kwenye ligi unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa
Ushirika, Moshi baada ya ule wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa ubao kusoma
Simba 2-0 Polisi Tanzania.
Akizungumza na Spoti Xtra, Meneja wa Simba, Patrik Rweyemamu
alisema kuwa maandalizi ya kikosi kwa mechi ambazo zimebaki yapo vizuri.
“Tupo vizuri kwa ajili ya mechi zetu ambazo zimebaki na mchezo
wetu ujao pia tunaamini kwamba tutapambana ili kupata pointi tatu, mashabiki
watupe sapoti kwani timu ilianza mazoezi Juni 8,” alisema Rweyemamu.
Incomplete history
ReplyDeleteWhat
whom
When
where
Mwandishii hataa hujui kuaaa walii badilii uwanjaa
ReplyDelete