June 18, 2021


 UONGOZI wa Azam FC umeweka wazi kuwa mipango yao ni kuhakikisha wanamaliza Ligi Kuu Bara katika nafasi mbili za juu katika msimamo ukiwemo ubingwa katika msimu huu.

 

Azam hadi sasa ipo nafasi ya tatu huku ikiwa na pointi 60 katika msimamo wa ligi ikiongozwa na Yanga yenye pointi 64 huku kinara akiwa ni Simba wenye 67.

 

 Ofisa Habari wa timu hiyo, Thabit Zakaria alisema kuwa upo uwezekano mkubwa kwao kupata nafasi ya pili kama watakosa ubingwa wa ligi.

 

“Maandalizi ya kumalizia mechi zetu zilizobaki bado yanaendelea kama kawaida na lengo letu ni kuhakikisha tunachukua nafasi ya pili kama tutakosa kuchukua ubingwa wa msimu huu.

 

"Kwa upande wa kikosi kipo salama kambini isipokuwa baadhi ya wachezaji ambao waliumia katika mchezo wa kirafiki Never Tigere na Bryson Raphael lakini pia na Prince Dube ambaye ana malaria,” amesema Zakaria.


Mtambo wao wa mabao ndani ya ligi ni Prince Dube ambaye ametupia mabao 14 na pasi tano za mabao akiwa ni namba moja kwa utupiaji Bongo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic