June 18, 2021


 BEKI wa pembeni wa Kagera Sugar, David Luhende, amekubali kukaa meza moja na mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya kujiunga na timu hiyo, huku akisema ana uhakika wa namba kwenye kikosi hicho.

 

Hiyo ikiwa ni siku chache tangu tetesi zizagae za beki huyo anayecheza upande wa kushoto nafasi inayochezwa na Mohammed Hussein ‘Zimbwe’ kutakiwa na Simba.

 

Simba imepanga kukifanyia maboresho kikosi chao katika baadhi ya nafasi ikiwemo ya ulinzi, kiungo na ushambuliaji katika kuelekea msimu ujao wa ligi.

 

 Luhende alisema kuwa yeye ni mchezaji huru ambaye mkataba unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu, hivyo anaruhusiwa kuzungumza na timu nyingine itakayomuhitaji.

 

Luhende alisema kuwa bado viongozi wa Simba hawajamfuata rasmi kwa ajili ya mazungumzo, lakini yeye yupo tayari kujiunga na timu hiyo kama wakifikia muafaka mzuri.


Aliongeza kuwa anaamini kiwango chake, hivyo ana uhakika mkubwa wa kuanza kucheza katika kikosi cha timu hiyo.



 

“Mimi maisha yangu yanategemea soka, hivyo nipo tayari kujiunga na timu yoyote itakayonihitaji, lakini kitu kikubwa nitakachokiangalia ni maslahi pekee.

 

"Hivyo niikaribishe Simba na timu nyingine itakayohitaji huduma yangu kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya awali kabla ya kusaini mkataba kwa makubaliano mazuri, naamini pale Simba mimi naweza kucheza,”alisema Luhende mwenye asisti saba msimu huu.

5 COMMENTS:

  1. Ni beki mzuri sana asiyeimbwa kwenye media.

    ReplyDelete
  2. Msijidanganye.....hana uwezo wa kusajiliwa Simba,ni beki wa kawaida tu ila kama kawaida ya kijarida hiki ni kuwapamba wachezaji ili wavute cha juu

    ReplyDelete
    Replies
    1. acha utani weweee
      Luhende ni moja ya mbavu bora za kushotoo hapa kwenye ligi yetuu
      wenzie ni Zimbwe, Kangwa, Manyama,
      narudia tena bonge la fullbek

      Delete
    2. Umeanza kumfuatilia lini?,uwezo wake ni wa kawaida tu.Hana nafasi Simba....nasisitiza

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic