June 9, 2021


 KOCHA wa timu ya taifa ya Ujerumani, Joachim Low amesema kuwa timu yake imeimarika sana baada ya kupata ushindi wa mabao 7-1 dhidi ya Latvia.

Ujerumani ilipata ushindi huo kwenye mchezo kirafiki juzi wakati timu yake ikijiandaa na michuano ya Euro.

Ujerumani haipewi nafasi kubwa ya kufanya vizuri kwenye michuano ya mwaka huu ilifanikiwa kwenda mapumziko ikiwa inaongoza kwa mabao 5-0.

"Sasa tupo vizuri, nafikiri matokeo haya yanaonyesha kuwa tunaweza kuwa vizuri huko tunapokwenda kwa kuwa tuna nia ya kufanya hivyo hiki ni kikosi bora," amesema.

Mabao ya Ujerumani kwenye mchezo huo yalifungwa na Gosens, Gundogan, Thomas Muller na Serge Gnaby huku Roberts Ozols akijifunga mengine yalifungwa na Timo Werner na Leroy Sane.

Huku Latvia wao wakiweka bao lao kambani kupitia kwa Die Mannschaft.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic