June 9, 2021


 UONGOZI wa Yanga umesema kuwa hali ya kiungo wao Tonombe Mukoko, ambaye alipata majeruhi akiwa kwenye majukumu ya timu ya taifa kwa sasa inaendelea vizuri.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa walipata taarifa kuhusu kuumia kwa mchezaji wao.

Bumbuli amesema:-“Tulikuwa na wasiwasi juu ya hali ya mchezaji Mukoko Tonombe ambaye aliumia kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Tunisia.

“Ila kwa sasa tumepata taarifa kwamba anaendelea vizuri na tumewasiliana naye kama klabu na hatua inyofuata ni madaktari kuzungumza na madaktari wa huko ili kujua kwamba kama anaweza kukaa nje kwa muda gani,” amesema Bumbuli.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic