June 3, 2021


 BEKI wa kikosi cha AS Vita Djuma Shaban amekubali kujiunga na Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nassredine Nabi.

Beki huyo raia wa Congo anatajwa kumalizana na mabosi wa Yanga ambao wapo kwenye mchakato wa maboresho wa kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nassredine Nabi.

Ikiwa mambo yatakuwa hivyo basi Julai Djuma atatangazwa kujiunga na kikosi hicho akiwa ni mchezaji huru.

Nyota huyo amesema:"Nimeambiwa kwamba Yanga wanahitaji huduma yangu, mimi sina tatizo ikiwa kutakuwa na makubaliano mazuri nitajiunga na kufanya nao kazi. Suala hilo nimeliacha mkononi mwa uongozi," .

Kwa mujibu wa meneja wa Djuma Faustino Mukandila amesema kuwa wapo kwenye mazungumzo na mabosi hao ambao wameonyesha nia ya kumpata beki huyo.

"Yanga wameonyesha nia ya kuhitaji huduma ya beki wetu hivyo kwa sasa tupo kwenye mazungumzo na ambapo tumefikia sio pabaya kila kitu kikiwa sawa tutaweka wazi," amesema.

Beki huyo pia alikuwa anatajwa kuwa kwenye mazungumzo na timu yake ili kumuongezea mkataba kwa kuwa bado wanahitaji saini yake.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic