NYOTA wa kikosi cha Simba, Perfect Chikwende inaelezwa kuwa huenda akaondolewa ndani ya kikosi hcho kutokana na kushindwa kuonyesha makeke ambayo walitarajia.
Ingizo hilo jipya kutoka FC Platinum alikuwa maalumu kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu Bara lakini ameshindwa kuwa chaguo la kwanza mbele ya Kocha Mkuu, Didier Gomes kwa kuwa mambo yamekuwa magumu kwake.
Habari kutoka Simba zinaeleza kuwa mpango wa kwanza ulikuwa ni kuvunja mkataba wa nyota huyo ila mambo yamekuwa magumu baada ya kuona gharama zitaongezeka.
"Chikwende hana nafasi kwa sasa ndani ya Simba ila ishu ni kwamba kama wanahitaji kuvunja mkataba wake gharama ni ndefu sasa hapo kwenye mkwanja ndo wanajadili.
"Ila kuna nafasi ndogo kwake kubaki kwani bado anaonekana hayupo kwenye mipango ya Gomes hivyo yupoyupo tu kwa sasa," ilieleza taarifa hiyo.
Chikwende alichukua nafasi ya Francis Kahata ambaye mkataba wake ulipomeguka hakupewa dili jipya zaidi ya mkono wa kwa heri.
Katika nafasi yake ya kiungo mshambuliaji ametengeneza pasi moja ya bao kati ya mabao 64 yaliyofungwa na Simba.
Hivi karibuni, Gomes alisema kuwa wachezaji wake wote wapo vizuri ila watakaofanya kazi kubwa kwenye mazoezi wana nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza.
Mikiaaa syndrome
ReplyDeleteMikia inakungojeeni hapo 3July ila mkiingia mitini kama walivotishia wazee wenu wa kazi kwa kisingizio cha kuonewa na kuzarauliwa
ReplyDeleteKwani mechi 2 zilizopita ilikuwaje ?
Deletekuna ya 4-1 na draw ya moja moja
Delete