MASAU Bwire, Ofisa Habari wa Ruvu Shooting ameweka wazi kwamba kuelekea kwenye mchezo wao wa ligi dhidi ya Yanga watapambana kupata matokeo chanya ili kurejea kwenye reli kwa kuwa hawapo sehemu salama.
Leo, Juni 17, Uwanja wa Mkapa unatarajiwa kuchezwa mchezo wa mzunguko wa pili ambapo ule wa mzunguko wa kwanza uliochezwa hapo ubao ulisoma Yanga 2-1 Ruvu Shooting.
Akizungumza na Saleh Jembe, Masau Bwire ambaye ni Ofisa Habari wa Ruvu Shooting amesema kuwa wanauhakika wa kufanya vizuri mbele ya Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nassredine Nabi raia wa Tunisia.
“Hapa sisi Ruvu Shooting tunaweka wazi kwamba mchezo wetu mbele ya Yanga ni muhimu kwetu kushinda ili turudi kwenye reli. Wachezaji wapo vizuri na maandalizi yapo sawa kwetu.
“Hatutaki kuwa sehemu ambayo wengi wanafikiria tutakuwa msimu ujao hivyo kazi ni moja tu kushinda mechi zetu ambazo zimebaki na hilo lipo wazi, mashabiki wasiwe na mashaka nasi.
"Wajitokeze kwa wingi kuona namna ambavyo tutafanya kwani kila kitu kipo sawa na mipango ipo kamili tunahitaji pointi tatu za Yanga," amesema Bwire.
Kwenye msimamo wa ligi, Ruvu Shooting ipo nafasi ya 10 na pointi 37 inakutana na Yanga iliyo nafasi ya pili na pointi 61.
Kuweni wanamichezo Mpira wa miguu siyo kamali , kwani walisubiri mechi ya Ya ga
ReplyDeleteUsiwe na waswas Mkwasa hawezi kututupa. Nina imani atafanya mipango hadi goli 3.
ReplyDeleteKama mikia inavyobebwa na KARIA,Board ya Ligi na Azam,KMC Namungo ya Pm nk
ReplyDelete