June 17, 2021


SERGIO Ramos, fundi wa mpira anatarajiwa kuondoka ndani ya kikosi cha Real Madrid baada ya kuwatumikia mabosi hao wa Hispania kwa muda wa miaka 16.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 35 ni nahodha pia wa kikosi hicho ni beki mwenye uwezo mkubwa ndani ya uwanja mchezo wake wa mwisho akiwa na jezi ya Real Madrid ulikuwa ni ule wa Ligi ya Mabingwa Ulaya ambapo walipoteza kwa kufungwa mabao 2-0 mbele ya Chelsea.

Mkataba wa Ramos ndani ya Santiago Bernabeu unameguka mwezi Juni na alipewa dili la mwaka mmoja ambao ulikuwa na makato ya mkwanja kutokana na mtikisiko wa uchumi uliosababishwa na janga la Corona jambo ambalo limemfanya nyota huyo agomee kuongeza mkataba kwa sababu alikuwa anahitaji mkataba wa miaka miwili na mkwanja mrefu.



Ameshinda mataji manne ya European Cups, mataji manne ya Kombe la dunia kwa Klabu, mataji matatu ya European Super Cup, mataji matano ya ligi, mataji mawili ya Copa del Reyes na anaondoka akiwa ni miongoni mwa wachezaji wenye historia matata ndani ya kikosi hicho nyuma ya Paco Gento.

Pia nyota huyo alienguliwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Hispania kinachonolewa na Kocha Mkuu, Luis Enrique kinachoshiriki Euro 2020 kutokana na kusumbuliwa na majeraha. Mbadala wa Ramos anatajwa kuwa ni David Alaba ambaye alijiunga na timu hiyo bure akitokea Klabu ya Bayern Munich.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic