June 5, 2021


FRANCIS Kahata, aliyekuwa kiungo wa Simba amewaaga mashabiki wake pamoja na viongozi baada ya kandarasi yake kuisha.

Kahata jina lake lilitolewa kwenye orodha ya nyota watakaoshiriki Ligi Kuu Bara na kuwa kwenye orodha ya wachezaji Li ya Mabingwa Afrika ambapo nafasi yake ilichukuliwa na kiungo Perfect Chikwende.

Baada ya timu ya Simba kuishia hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa dili la Kahata likawa limeisha na mabosi wa Simba hawakuwa na mpango wa kumuongezea dili jingine.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Kahata amesema:"Asanteni Wanasimba kwa sapoti, benchi la ufundi pamoja na wachezaji, najivunia muda wangu ndani ya timu hii na mafanikio niliyoyapata.

"Ilikuwa safari yenye kumbukumbu tamu na chungu. Ni wakati wa kutafuta changamoto nyingine, asanteni na mpaka wakati mwingine.” .

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic