UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa wengi katika mechi zao ambazo zimebaki watapambana kupata ushindi kwa kuwa wapo imara.
Ndani ya Ligi Kuu Bara, Yanga imecheza jumla ya mechi 29 ina pointi 61 vinara wa ligi ni Simba wakiwa na pointi 64 baada ya kucheza jumla ya mechi 67.
Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa mechi nne zilizopo kwenye ratiba hizo mwalimu ameshaanza mbinu tayari kiufundi huku ule wa kiporo dhidi ya Simba unaotarajiwa kuchezwa Julai 3 maandalizi yake yamekwisha.
“Kwenye mechi zetu nne ambazo zipo kwenye ratiba hapo hesabu zetu ni kuona kwamba tunashinda na ipo wazi hata mwalimu mwenyewe anajua. Ila hiyo ya Julai 3 dhidi ya Simba maandalizi yake yamekwisha na kiporo hakihitaji mambo mengi muda wowote sisi tupo tayari kucheza na Simba,” amesema Bumbuli.
Mechi za Yanga ambazo zimebaki kwa sasa ni dhidi ya Ruvu Shooting Juni 17, Mwadui FC Juni 20, Simba, Julai 3, Ihefu FC, Julai 13 na Dodoma Jiji, Julai 18.
Simba amecheza mechi 67? Rekebisha bwana
ReplyDeleteHawana muda wa kuhariri, hata points walizosema za Simba sio sawa!
DeleteHapo ubingwa wameusahau kuutaja
ReplyDeleteMara mechi ya july 3 hamuitambui, Mara maandalizi tayari.. hamueleweki
ReplyDelete