WILLIAM Gallas, raia wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 43 anaamini kuwa, Kocha Mkuu, Mikel Arteta hakuwa tayari kuinoa Arsenal.
Arsenal ilimpa kazi raia huyo wa Hispania baada ya kumfungashia virago, Unai Emery. Mafanikio ambayo ameyapata Arteta ndani ya Arsenal ni kutwaa taji la FA msimu wa 2019/20.
Msimu wake kamili wa 2020/21 imeshuhudiwa Arsenal ikimaliza nafasi ya nane kwenye msimamo na itakosa michuano ya Ulaya kwa mara ya kwanza baada ya kuyeyuka miaka 25.
Nyota huyo alicheza ndani ya kikosi hicho kuanzia 2006-2010 anaamini kwamba Arteta hakuwa tayari kupewa kazi hiyo kubwa katika kuitumikia Arsenal.
"Mikel Arteta bado hakuwa tayari kuiongoza timu kama Arsenal. Sawa alikuwa kocha msaidizi Manchester City. Lakini hakuwahi kuongoza timu hiyo ni tofauti kabisa," .
0 COMMENTS:
Post a Comment