June 28, 2021


ANAANDIKA Haji Manara Ofisa Habari wa Simba namna hii:- Sitegemei kusikia mizengwe ya wale waliokuwa wakikesha katika redio kupinga mabadiliko ya uendeshaji wa vilabu.


Yoyote mwenye kutaka mafanikio ya vilabu vyetu lazma aunge mkono mabadiliko ambayo Simba na Yanga wanavyotaka kuyafanya.

Wale waliokuwa wakiwatumia wapinga mabadiliko ya Simba na kuwaita kila siku kuwahoji tunawaomba wasifanye hivyo kwa wenzetu.

Na hatutegemei kuona simu zao kila siku kwenda FCC kuhoji mizengwe isiyo na faida yoyote kwa vilabu vyetu. Waache Wanachama walioamua kubadilisha mifumo wakamilishe dhamira zao njema.



Isije tena watu wale wale kuanza kutumika kuvuruga hivi vilabu kwa maslahi yao, maana huko wenzetu mna vigogo viwili, ikitokea mmoja akaslide kidogo tu,basi mtawaona wapika sumu!.

Hao hawakawii kuvuruga mambo, walau Simba ilishawachukulia kama machale tu, sasa nyie Yanga kaeni nao macho hao watu, hawana dini katika Bakhshishi na wapo tayari kufanya lolote lile ili mradi yao yatimie.

Ahhh tuachane na hayo, mimi nawatakia kila la kheri Watani zangu katika mabadiliko mliyoyaanza jana, najua huo ni mwanzo kwa vilabu vyote nchini kwenda na mifumo ya kisasa ya uendeshaji wa vilabu vya soka wenye tija kwetu.

9 COMMENTS:

  1. Nyundo ya utosini kwa wale waandishi takataka

    ReplyDelete
  2. Binamu yangu leo umeongea point ambazo unaweza kuombea mkopo Benki ya Dunia au hata kwa Bill Gates.

    ReplyDelete
  3. Yanga ikiwa strong inaifanya simba kuwa strong vivyo hivyo simba ikiwa strong inaifanya yanga nayo kuwa strong,ifikie wakati hizi club mbili kubwa kwenye ukanda huu wa Africa mashariki na kati ziwe zina supportiana kwa maendeleo ya nchi yetu na ukanda wetu sio kila siku kuoneana wivu na chuki zisizo na maana,mie ni mpenzi wa mnyama ila Haji ungekuwa unatoa kauli kama hizi kwa sehemu zingisaidia sana pia wadau wengine wangejifunza kitu kwako,sio kila kukicha iwe ni matusi weeeeee

    ReplyDelete
  4. Niseme ukweli. Tatizo ni viongozi majizi walioonhoza yanga
    Wamekuwa wakikitumia kichaka cha chuki baina sisi na simba kuficha wizi wao dhuluma dhidi wa wavhezaji, dhuluma dhidi ya makocha. Na maovu mengi. Lakini sasa tumeshasajua.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Watu kama nyie ndo aliowazungumzia Haji Manara,ukiambiwa utoe ushahidi utaanza kuweweseka,nina hakika hauna mchango wowote katika klabu zaidi ya majungu kama hayo uliyoyaandika

      Delete
  5. Bila ya Simba na watani Yanga, hakuna msisimko wa kandanda kwa hivo ni lazima tuzitaki kila la kheri timu hizo na zote nyengine zilizobaki

    ReplyDelete
  6. Hakki ya MUNGU yaani leo nimefurahi sana maana afadhali tunaanza kujua nini maana ya uzalendo na nini maana ya utani wa jadi ahasanteni watanzania munaojielewa tuendelee hivi hivi tusibadilike TUTANIANE NA TUSIGOMBANE NA KUTUKANANA

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic