June 19, 2021


NAHODHA wa timu ya taifa ya England, Harry Kane amebebeshwa mzigo wa lawama kwa kushindwa kuonyesha uwezo mkubwa katika mchezo wa Euro 2020 wakati akiwa na timu ya taifa ya Engand ilipopambana na timu ya taifa ya Croatia.

Kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Wembely dakika 90 zilikamilika na ubao huo ukisoma England 0-0 Croatia ambazo zote zipo katika kundi D linaloongozwa na Czech Republic yenye pointi 4 na mabao matatu huku England ikiwa nafasi ya pili na pointi 4 imetupia bao moja.

 Croatia ipo nafasi ya tatu na pointi moja sawa na Scotland iliyo nafasi ya nne zote zikiwa zimecheza mechi mbilimbili.

Mchambuzi wa masuala ya michezo, Roy Keane ameiambia ITV kwamba Harry Kane alionekana akiwa amekosa spidi na nguvu ya kupambana kwa ajili ya timu yake ya taifa ya England jambo ambalo limemfanya ashindwe kuonyesha ushindani kwenye mchezo huo.

Katika mchezo huo rekodi zinaonyesha kuwa Kane aligusa mpira mara 19 ikiwa ni idadi ndogo kuweza kufanya kwake akiwa na timu ya taifa na licha ya kwamba ni mshambuliaji alishindwa kupiga hata shuti moja ambalo lililenga lango la wapinzani.


"Harry Kane anaonekana kama kuna vitu vimembadili hivi. Yupo lakini hana ile spidi hayupo fiti katika miguu muda wote. Ikiwa England wanahitaji kushindana katika mashindano haya lazima wawe na mtu ambaye anakubali kujitoa na kupambana muda wote," amesema Roy.



2 COMMENTS:

  1. Kama samata na stars

    ReplyDelete
  2. Ubelgiji bhana ndio kuna watu wanajua kujitoa atleast na ujeruman maana hata huyo france alijiuliza maswali mengi sana kapataje matokeo? Uingereza hakuna kitu pale na kombe litagombaniwa na ujeruman,italy, ubelgiji, szech republic, portugal sweden, netherland labda na huyo france hizo ndizo timu zitakazofika mbali sana msimu huu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic