June 19, 2021


MZAWA Feisal Salum amepachika mabao mawili ndani ya kikosi cha Yanga baada ya kuyeyusha muda wa siku 176 ambazo ni sawa na saa 4,224.

Kiungo huyo mara ya mwisho kufunga bao ndani ya ligi ilikuwa ni Desemba 23 mbele ya Ihefu ambapo alipachika bao moja dakika ya 59 baada ya hapo alishindwa kufurukuta kwa kutoa pasi ya bao wala kufunga katika mechi 10 ambazo alicheza.

 Kwenye mechi hizo Fei alitumia jumla ya dakika 831 zote ziliyeyuka bila kufunga licha ya kuwa ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Nassredine Nabi.

Mechi ambazo alicheza bila kufunga wala kutoa pasi ya bao ilikuwa mbele ya Tanzania Prisons ilikuwa Desemba 31, Mbeya City ilikuwa ni Februari 13,  Kagera Sugar ilikuwa ni Februari 17,  Mtibwa Sugar, Februari 20.

Coastal Union , ilikuwa ni Machi 4, Polisi Tanzania, Machi 7, KMC, Aprili 10, Azam FC ilikuwa Aprili 25, Namungo Mei 15, JKT Tanzania, Mei 19.

Kwenye msimamo wa ligi, Yanga imefikisha jumla ya mabao 46 baada ya kucheza mechi 30 ipo nafasi ya pili na vinara ni Simba wenye pointi 67 baada ya kucheza mechi 27.

3 COMMENTS:

  1. Wewe sema magoli ya kufundishwa

    ReplyDelete
  2. Michezo mingi amecheza namba 6 au 8, Juzi kapangwa namba 10, ni majukumu tu anayopewa na makocha wake

    ReplyDelete
  3. Masaa mangapi??? Duh! Haaa haaa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic