June 30, 2021


 WAKATI tetesi zikieleza kuwa kiungo wao fundi wa kutumia mguu wa kushoto kufunga Luis Miquissone yupo kwenye rada za Yanga uongozi wa Simba umesema kuwa bado dili hilo halijakamilika na mkwanja unaohitajika ni mrefu.

Ndani ya ligi, Luis akiwa ametupia mabao 9 amefunga mabao 7 kwa mguu wa kushoto huku moja akitumia mguu wa kulia na lingine alifunga kwa kichwa dk 90 mbele ya Tanzania Prisons, Uwanja wa Mkapa.

Haji Manara Ofisa Habari wa Simba amesema kuwa hakuna taarifa yoyote kuhusu mchezaji huyo kuuzwa na badala yake timu itakayomhitaji lazima itoe mkwanja mrefu kupata saini yake.

"Hakuna ambaye anaweza kusema kwamba mchezaji wa Simba ni mali yao kwa sasa, hakuna tetesi za namna hiyo eti unasema mchezaji anatakiwa na timu fulani wakati bado ana mkataba?

"Kuna mob ambayo inapenda kwenda na mambo hasa yanapotokea na tunayajua ila sio kwa hili hakuna jambo kama hilo, Simba tupo tofauti kabisa, ikiwa kuna timu kutoka Tanzania inamuhitaji Luis ijiandae kutoa dola milioni 10," amesema.

Mbali na abao 9 ambayo amefunga kwenye ligi pia Luis ametoa jumla ya pasi 10 za mabao kwa msiu wa 2020/21.

5 COMMENTS:

  1. Kwa Nanji dola mil 10 sio kitu. Mwakani miquisoni ni wetu yanga. Simba poweni moto. Hakuna ubaya mchezaji ku cross

    ReplyDelete
  2. Kati ya Mo na Manji nani mwenye pesa zaid?

    ReplyDelete
  3. Manji keshafilisika hawezi kutumia 10m US $ kwa mchezaji hilo sahau. Msitupe mbachao(hsm) kwa msala(manji) upitao

    ReplyDelete
  4. ntawaona wajinga sana simba kama huu mkataba utakuwa na mapungufu pia ntamuona miquissone mjinga sana kama atakubali kuhamia timu zingine za hapa tanzania

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic