MKATA umeme na nahodha wa zamani wa klabu ya Arsenal, Patrick
Vieira yupo kwenye mazungumzo na klabu ya Crystal Palace ili kuchukua nafasi ya
Roy Hodgson kama kocha mpya wa timu hiyo.
Inaelezwa kuwa mpaka sasa tayari mazungmzo ya pande hizo
mbili yamekamilika kwa asilimia 75.
Palace wamefikia maamuzi hayo baada ya kushindwana na kocha, Nuno Espirito Santo, huku ofa yao kwa kocha Lucien Favre ikipigwa chini mapema mwezi huu.
Vieira, ambaye alifutwa kazi na klabu ya Nice mwezi Desemba
mwaka jana, anatajwa pia kuchukua majukumu ndani ya kikosi cha Selhurst Park.
Kwa sasa nyota huyo wa zamani wa Arsenal anafanya kazi kama
mchambuzi wa soka katika kituo cha ITV cha Uingereza kama mchambuzi wa michuano
ya Euro 2020.
0 COMMENTS:
Post a Comment