NAHODHA wa Klabu ya Simba, John Bocco leo Juni 15 amekabidhiwa tuzo yake ya mchezaji bora wa mwezi Mei.
Nyota huyo mwenye mabao 13 ndani ya Ligi Kuu Bara alipata tuzo hiyo baada ya kuwashinda wachezaji wenzake aliotinga nao fainali.
Alikuwa ni Bernard Morrison kiungo mshambuliaji na Taddeo Lwanga kiungo mkabaji.
Tuzo hiyo ni maalumu kwa ajili ya kuwapa motisha wachezaji wa Simba kupambana na inaitwa tuzo ya mashabiki ambayo inadhaminiwa na Emirate Aluminium Profile na hutoa milioni moja kwa mshindi.
Kura za mshindi hupatikana kwa mashabiki wa Simba kupiga kupitia tovuti ya Simba.
0 COMMENTS:
Post a Comment