June 7, 2021


 MSHAMBULIAJI wa Juventus, Alvaro Morata amedai kuwa yeye ni mmoja wa wachezaji wanaomjua vizuri mshambuliaji mwenzake, Cristiano Ronaldo.

 

Morata ambaye amecheza na Ronaldo pia Real Madrid, amesema kuwa nyota huyo ni mtu anayejua mambo mengi ambayo watu wanaweza wasifikirie kama anayajua.

 

“Huwa tunazungumza mambo mengi, mengine hata ambayo huwezi kuyafikiria. Anajua vitu vingi mfano historia na rekodi mbalimbali, inaonekana kama anasoma sana vitabu.

 

“Kuna siku tukiwa tunakula katika timu, akachambua mambo kadhaa kuhusu chakula kisha akatutajia mtu ambaye aliwahi kukaa muda mrefu bila kula. Ilitushangaza wote,” alisema Morata.


Mshindani wake mkubwa ambaye ni mshikaji wake pia ni Lionel Messi wa Barcelona.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic