BAADA ya Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) kupitia kikao chao cha Juni 24,2020 kupitia mwenendo wa matukio mbalimbali ya Ligi Kuu Bara, Ligi Daraja la Kwanza kufanya maamuzi yao ni rasmi kuwa kipa namba moja wa Yanga Metacha Mnata atakosekana kwenye mchezo dhidi ya Simba.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Julai 3, Uwanja wa Mkapa na unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote mbili.
Kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Juni 17, wakati ubao wa Uwanja wa Mkapa ukisoma Ruvu Shooting 2-3 Yanga Mnata alionyesha ishara ya matusi kwa mashabiki.
Kutokana na kosa hilo ametakiwa kulipa faini ya laki tano kwa kosa hilo lililosababisha hasira kwa mashabiki.
Pia Ruvu Shooting imepewa onyo kwa kosa la kuingiza gari la kubeba wagonjwa kwenye njia ya kukimbilia.
Pia timu ya Tanzania Prisons imepewa onyo kali kwa kosa la kutoingia kwenye chumba chao cha kubadilishia nguo kwa madai kuwa kilipuliziwa dawa na ripoti ya daktari wa mkoa ilieleza kuwa hakukuwa na dalili zozote za kuonekana kwamba hewa imechafuliwa.
Ilikuwa ni kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Kaitaba, Juni 16 na ubao ulisoma Kagera Sugar 1-0 Prisons.
Metacha kafungiwa mechi ngapi? Waandishi mnakwama wap
ReplyDeleteWaandishi hawa ni sheeeda wanakwama parefu mno 🤣🤣
DeleteKwa Metacha hakipungui kitu. Ila bado nina wasiwasi timu yetu ni dhaifu mbele ya simba.
ReplyDelete