June 5, 2021


INJINIA Hersi Said, ambaye ni Mkurugenzi wa Uwekezaji ndani ya Kampuni ya GSM na Makamu Mweyekiti wa Kamati ya Usajili wa Yanga amesema kuwa wamefanikiwa kufanya maendeleo makubwa kwa msimu huu ikiwa ni pamoja na kutwaa taji la Kombe la Mapinduzi.

Chini ya Kocha Mkuu, Cedric Kaze ambaye alifutwa kazi kutokana na kile kilichoelezwa kuwa mwendo mbovu ilifanikiwa kutwaa taji hilo.

Katika fainali iliyofanyika Zanzibar, Yanga ilishinda kwa penalti 4-3 dhidi ya Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes ila zama za Mapinduzi ilikuwa mikononi mwa Seleman Matola ambaye ni kocha msaidizi.

Injinia amesema:"Yanga ime-archieve(fanikiwa) vitu vikubwa, tumechukua ubingwa wa mapinduzi, naamini wote mnaamini ni heshima kubwa.

"Haya ni mapinduzi halali yanaitwa Mapinduzi ya Zanzibar.

"Tumechukua ubingwa wa Mapinduzi mbele ya watani zetu wa jadi wakubwa, kwangu ni succes, (mafanikio) ambayo hatujapata miaka miwili iliyopita.

"Pia kwa sasa timu ipo nusu fainali ya Kombe la Shirikisho tunakwenda kufanya vizuri na tutafanya vizuri nina amini katika hili,". 

2 COMMENTS:

  1. Kweli maendeleo mkubwa sana kutokana na na msimu huu na bado makombe yanakuja nalo ubingwa na jinsi ya kuheshimu kanuni tukaingia mitini kuepukana na hatari za mikia pamoja na kutimuwa mako ha watatu mmojaapo alietupa kombe la mapinduzi na mengi menginefff

    ReplyDelete
  2. Neno sahihi hapo ni "achieve", sio "archieve". Kuweni makini kwy proofreading.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic