June 18, 2021


 LICHA ya mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere kupitia kipindi kigumu cha kukosa nafasi ya kuanza mara kwa mara kwenye kikosi cha kwanza, kocha wa viungo wa timu hiyo, Adel Zrane amesema kuwa mshambuliaji huyo bado ana nafasi kubwa ya kufanya vizuri ndani ya kikosi cha Simba.

 

Tofauti na misimu miwili iliyopita, Kagere msimu huu amekuwa na wakati mgumu kupata nafasi ya kuanza mara kwa mara kwenye kikosi cha kwanza, kutokana na ushindani mkubwa wa namba anaoupata kutoka kwa washambuliaji Chris Mugalu na John Bocco.

 

Licha ya changamoto hiyo ya nafasi Kagere msimu huu mpaka sasa kwenye michuano ya Ligi Kuu Bara pekee, amefanikiwa kuifungia Simba mabao 11 yanayomuweka katika nafasi ya tatu ya msimamo wa chati ya wafungaji bora msimu huu.


Akizungumza na Championi Jumatatu, kocha Zrane alisema: “Kwangu Kagere ni miongoni mwa washambuliaji bora zaidi katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na kati, hili linathibitishwa na ukweli kwamba kwa misimu mitatu iliyopita amefanikiwa kuibuka na tuzo za ufungaji bora katika nchi tofauti.

 

"Lakini kwa mchezaji kuna wakati unaweza kukutana na changamoto ya kiwango chako au hata ya kimfumo, lakini binafsi namjua Kagere vizuri na kutocheza kwake kwa sasa haimaanishi kuwa ni mchezaji mbaya, nina uhakika Kagere bado ana nafasi ya kufanya makubwa akiwa na kikosi cha Simba, hilo ni suala la muda tu.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic