June 19, 2021


HASSAN Bumbuli, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa nyota wao wawili ambao ni Farid Mussa na Mukoko Tonombe wanaendelea vizuri.

Bumbuli amesema:"Hali za wachezaji kwa sasa ni nzuri tunamshukuru Mungu kwamba wachezaji wanaendelea vizuri.

"Farid Mussa aliugua ghafla muda wa mapumziko hivyo alibadilishwa kutokana na kupata allergy (mzio) na madaktari wamesema kuwa anaendelea vizuri.

"Mukoko Tonombe anaendelea vizuri madaktrai wameshauri kwamba apewe muda wa uangalizi kwa kuwa huenda likawa ni lile tatizo ambalo alipata akiwa na timu ya taifa ya Congo.

Wachezaji hawa walipata maumivu kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Ruvu Shooting uliochezwa Uwanja wa Mkapa ambapo ubao ulisoma Ruvu Shooting 2-3 Yanga.

Kuhusu Yacouba Bumbuli amesema:-"Yacouba Songne amerejea na yupo kambini akiwa na wachezaji wakiwa kwenye maandalizi ya mechi yetu ijayo dhidi ya Mwadui FC," amesema.

Yanga kwenye msimamo wa ligi ipo nafasi ya pili imekusanya jumla ya pointi 64 baada ya kucheza jumla ya mechi 30 inakutana na Mwadui FC iliyo nafasi ya 18 na pointi 19.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic