June 7, 2021


NYOTA wa kikosi cha Simba, Bernard Morrison amesema kuwa alipanga kushangilia kwa mtindo mwingine kabisa ila alizuiwa na wachezaji wenzake pamoja na kocha.

Walipocheza na Namungo, Morrison alifunga bao bora kwake ambalo mashabiki wa Simba ikiwa ni pamoja na Aggy Simba alisema kuwa lile ni bao bora la msimu kwa kuwa alilipachika akiwa nje ya 18.

Baada ya kufunga bao hilo Morrison alishangilia kwa mtindo ambao hupendwa kutumiwa na nyota wa Namungo, Stephen Sey kwa mtindo wa kupunga.



Morrison amesema:"Nilipanga kushangilia kwa mtindo tofauti ila nilikatazwa na wachezaji wenzagu ikiwa ni pamoja na Erasto Nyoni, pia Zraine, (Adel ambaye ni kocha wa viungo) naye alinizuia pia.

"Nilifanya hivyo kwa kuwa nilimwambia awali kwamba lazima tutawafunga nami nilikuwa ninapambana kufunga kwa namna yoyote ilipotokea sikuwa na chaguo zaidi ya kupunga.

"Pia mimi na Sey wote ni marafiki kwa kuwa tunawasiliana na kuongea mambo mengi hivyo hamna tatizo kati yangu na yeye," amesema.

2 COMMENTS:

  1. Walimzuwua kusherehekea ili kupunguza ghadhabu za qarani lakini haijusaudua kitu na ndio siku yapilu wakazuwa tena kama ada tao kufunguwa kesi eti warejeshewe Morrison wao. Hahahaaaaa

    ReplyDelete
  2. Boya tu aache uongo eti alizuiwa. Hana jipya, asubiri msimu uishe na thamani yake iishe

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic