NYOTA wa kikosi cha Azam FC kinachonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Mei.
Mshambuliaji huyo ni kinara wa utupiaji ndani ya Ligi Kuu Bara akiwa na jumla ya mabao 14 kibindoni kwa sasa msimu wa 2020/21.
Dube ametwaa tuzo hiyo baada ya kuonyesha kiwango bora kabisa katika mechi za mwezi huo, akifunga mabao mawili katika mechi mbili na kuisaidia Azam FC kuvuna pointi zote sita dhidi ya KMC (2-1) na Biashara United (2-0).
Aliwashinda wachezaji wenzake wawili ambao ni Erick mwijage wa Kagera Sugar na kipa namba moja wa Yanga, Metacha Mnata.
Mbali na Dube pia Lwandamina ametwaa tuzo ya kocha bora mwezi Mei ambapo aliwashinda Francis Baraza wa Kagera Sugar na Abdalah Mohamed wa JKT Tanzania.
Safi sana Dube endelea kuwanyoosha,ila jipange kupambania kiatu maana huyo bocco kama kazaliwa upyaa,kagere nae hatabiriki,siku moja tu utashangaa anapiga tatu,tayari anakuacha.
ReplyDelete