June 7, 2021


 DICKSON Ambundo, nyota wa kikosi cha Dodoma Jiji kwa sasa anawasubiri Yanga ili aweze kusaini dili jipya kwa kuwa kandarasi yake inameguka na bado hajaongeza mkataba kwenye timu yake ya sasa inayonolewa na Kocha Mkuu, Mbwana Makata kwa mujibu wa ripoti.


Mtu wa karibu wa Ambundo ameliambia Spoti Xtra kuwa mpaka sasa hakuna kiongozi wa Yanga ambaye ameufuata uongozi wa timu hiyo licha ya tetesi kueleza kwamba yupo kwenye mazungumzo ya awali.


“Ambudo yupo na timu yake na anachosubiri kwa sasa ni kuona kama viongozi wa Yanga watamfuata kwani zote ni tetesi na hakuna ambaye amezungumza naye hivyo ni suala la kusubiri kwani mchezaji mwenyewe anawasubiri Yanga ili amalizane nao,” ilieleza taarifa hiyo.


Akizungumza na Spoti Xtra, Ambundo alisema kuwa hawezi kuzungumzia kuhusu tetesi kwa kuwa bado yupo ndani ya Dodoma Jiji hivyo kama kuna timu inamuhitaji ifuate utaratibu.


“Nipo na Dodoma Jiji kwa sasa ikiwa kuna timu ambayo inahitaji huduma yangu ni suala la kuzungumza na uongozi wangu, mimi nitapewa taarifa kwani kazi yangu ni kucheza,” .

Nyota huyo amecheza pia ndani ya Alliance FC ya Mwanza ambayo kwa sasa ina uhakika wa kushiriki Ligi Daraja la Pili pia aliwahi kucheza Gor Mahia ya Kenya.





0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic