June 17, 2021


 MSHAMBULIAJI namba mbili ndani ya Simba, Meddie Kagere rekodi zinaonyesha kwamba ujanja wake ni kwenye viwanja viwili msimu huu wa 2020/21.

Ujanja wake ni kwenye Uwanja wa Mkapa na Uwanja wa Jamhuri kwa kuwa ametupia mabao mengi kila anapopata nafasi ya kucheza kwenye viwanja hivyo viwili tofauti na akicheza katika uwanja mwingine.

Kibindoni ametupia jumla ya mabao 11 na namba moja kwa utupiaji ndani ya Simba ni mzawa John Bocco mwenye mabao 13 huku Prince Dube wa Azam FC akiwa ni namba moja kwa watupiaji wote akiwa ametupia mabao 14.

 Katika hayo mabao 11, ni matatu alitupia nje ya Dar ilikuwa mbele ya JKT Tanzania na alifunga mabao mawili pia alitupia bao moja mbele ya Dodoma Jiji ilikuwa ni kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.


Mabao nane alitupia Uwanja wa Mkapa ilikuwa mbele ya Biashara United, Gwambina , Azam FC, KMC ilikuwa ni mwendo wa mojamoja na mabao mawili alifunga mbele ya Ihefu na Mtibwa Sugar.


Kocha Msaidizi wa Simba, Seleman Matola amesema kuwa sababu kubwa ya wachezaji kushindwa kupeta kwenye viwanja vingi ni ugumu wa miundombinu ambayo wanakutana nayo.


"Kuna mazingira mengine inakuwa ngumu kwa wachezaji kucheza namna ambavyo wamezoea kutokana na ugumu wa miundombinu, lakini haina namna muhimu kwetu kupambana," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic