KIKOSI cha Yanga kitamachonolewa na Kocha Mkuu, Nassreddine Nabi leo Juni 17 kimesepa na pointi tatu mazima mbele ya Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Mkapa.
Wakati ubao ukisoma Ruvu Shooting 2-3 Yanga, Feisal Salum alianza kufungua akaunti ya mabao kwa wapinzani wao.
Ilikuwa ni dakika ya 23 na lile la pili alipachika dakika ya 32 na kuwafanya kwenda mapumziko wakiwa wanaongoza kwa mabao hayo.
Kipindi cha pili, Ruvu Shooting walianza kwa kasi na kupachika dakika ya 70 kupitia kwa Emmanuel Martin kisha Yanga walipata bao la ushindi dakika ya 80 kupitia kwa Saido Ntibanzokiza.
Ni David Richard wa Ruvu Shooting alipachika bao la kufuta machozi dakika ya 82 na jitihada zao kusaka pointi zilikwama baada ya dakika 90 kukamilika.
Ushindi huo unaifanya Yanga kufikisha jumla ya pointi 64 ikiwa nafasi ya pili huku Ruvu Shooting ikiwa nafasi ya 10 na pointi 37.
Tangu mkwasa akaifunga yanga, thubutu, huyo ni agent
ReplyDeleteKama walivyo Namungo kwa vimburu
DeleteYes mpe ukweli huyu
DeleteSaida mmepiga jiwe la kichwa kakosa nini?Utopolo mna lana.Ndio maana Metacha kawaonyesha cha kati.
ReplyDeleteSimba 3 Ruvu Shooting kikosi kamili 0
ReplyDeleteYanga kikosi kamili 3 Ruvu Shooting Kikosi kasoro 2.
Nani mwenye mkono wa juu hapo?
Matopolo chupuchupu jana wakitimuliwa na polisi kama ngedere kwa fujo lao
ReplyDelete