NYOTA wa kikosi cha Liverpool inayoshiriki Ligi Kuu England, Sadio Mane amecheza jumla ya mechi 229 na aliibuka ndani ya kikosi hicho akitokea Southampton msimu wa 2016/17.
Msimu huu wa 2020/21 ametupia mabao 11 na jumla ya pasi 7 katika mechi 35 ambazo amecheza na ana wastani wa kufunga kila baada ya dk 255.
Jumla katika mechi 229 amefunga mabao 95 na pasi za mabao ni 36 ndani ya mechi za Ligi Kuu England.
Msimu wake wa kwanza ndani ya Liverpool alianza kikosi cha kwanza mechi 27 na moja akitokea benchi na alitupia jumla ya mabao 13.
Pia ana tuzo moja ya mfungaji bora ambapo alitwaa msimu wa 2018/19 alitupia jumla ya mabao 22 katika mechi 36 alizoanza kikosi cha kwanza na mechi moja alianzia benchi.
Raia huyo wa Senegal amenyanyua mara moja taji la Ligi Kuu England akiwa na Liverpool ilikuwa msimu wa 2019/20 na jezi anayopenda kuivaa mshambuliaji huyo ni namba 10.
0 COMMENTS:
Post a Comment