June 26, 2021


 NYOTA wa kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes, Clatous Chama ameweka rekodi yake ya kuhusika kwenye jumla ya mabao 21 ambayo ni sawa na yale yaliyofungwa na timu nzima ya Coastal Union.

Akiwa ni namba moja kwenye kutengeneza pasi za mwisho akiwa nazo 13 pia amefunga mabao 8 jambo ambalo linaikuza thamani yake ndani ya Bongo.

Wakati Simba ikiwa imefunga jumla ya mabao 69 baada ya kucheza mechi 29 amekuwa na mchango mkubwa ambapo aliweza kuvunja rekodi yake aliyoweka msimu uliopita baada ya kufunga mabao mawili na kutoa pasi 10 za mabao.

Wakati Chama akifanya hivyo, timu ya Coastal Union inayonolewa na Kocha Mkuu, Juma Mgunda imefunga jumla ya mabao 21 kwenye msimamo ipo nafasi ya 17 na safu yake ya ushambuliaji ni namba moja kwa ubutu ikifuatiwa na Ihefu ambayo imefunga mabao 22 kwenye mechi 32.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic