June 5, 2021


 HESABU ambazo zinapigwa kwa sasa kwa timu zilizo nje ya 10 bora ni namna gani zinaweza kujinasua kwenye suala la kushuka daraja na hatimaye ziepuke kikombe cha kuweza kushiriki Ligi Daraja la Kwanza msimu ujao wa 2021/22.

Wakati wao wakifikiria hivyo basi kuna umuhimu wa Shirikisho la Soka Tanzania,(TFF) kufikiria pia namna bora ya kuwalinda wachezaji pamoja na ligi yao.

Wale ambao wanashiriki Ligi Daraja la Kwanza kwao kulia na suala la ukata ni jambo la kawaida na kulia kwamba wanaonewa na waamuzi ni jambo ambalo wanaishi nalo.


Sasa ikiwa kwa msimu huu kuna timu nne zinashuka kama ambavyo ilikuwa msimu uliopita kutoka ligi kuu,  basi kuna umuhimu wa kuboresha mazingira yao katika ligi ambayo watashiriki wakati ujao.

Kuanzia namna ya mfumo wao utakavyokuwa namna katika kucheza pamoja na kufuatiliwa basi iwe ni kwa ukaribu mkubwa ili kuweza kuongeza ushindani na huku pia.

Imekuwa kawaida kwa timu zote kutaka mechi zao zionyeshwe na Azam TV ila sasa kigezo kinakuja kwamba kila timu inahitaji kuona mechi yake ikiwa ugenini inaonyeshwa ila wao wakiwa nyumbani hawataki.

Hapo kuna jambo ambalo inabidi liwekwe sawa kisha hawa wamiliki wa timu pamoja na timu zote kukubaliana kwamba mechi zote na zionyeshwe wakati ujao.

Jambo ambalo lipo kwa sasa kwenye Ligi Daraja la Kwanza ni ushindani hasa kwa timu zinazotoka Ligi Kuu Bara kushindwa kwenda na kasi ambayo wanakutana nayo na mwisho wa siku wengine wamekuwa wakianguka mpaka Ligi Daraa la Kwanza.

Imekuwa hivyo hata msimu huu wakati Geita Gold na Mbeya Kwanza zikipanda Ligi Kuu Bara, Mbao, Alliance, Lipuli hizi zilikuwa ndani ya ligi msimu uliopita kisha zikashuka zimeshuka mazima mpaka Ligi Daraja la Pili.

Ninaamini kwamba ikiwa mazingira yataboreshwa na TFF kuongeza nguvu huku basi itakuwa rahisi kwa msimu ujao timu zote zikakubaliana kwamba mechi zote zionyeshwe na ushindani ukazidi kuwa mkubwa.

Pia wadau nao wasiweke kando timu shiriki Ligi Daraja la Kwanza na la Pili huku ni chimbuko la wachezaji pamoja na timu zijazo kwenye ligi.

Muhimu kuwa na ushindani huku wadau nao wakiwapa sapoti wachezaji pamoja na timu kiujumla katika utendaji wa kazi.

Kila kitu kinawezekana kikubwa ni mipango kazi safi na kila mmoja kutimiza wajibu wake kwa wakati.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic