LIONEL Messi, nyota wa Barcelona bado yupo sana ndani ya kikosi hicho baada ya kumalizana na mabosi wa timu hiyo kwa mujibu wa ripoti.
Habari zimeeleza kuwa Barcelona imefanya mazungumzo na Messi kuhusu kuongeza mkataba mpya kilichobaki kwa sasa kwa nyota huyo ni kumwaga wino ili kuhakikisha nafasi ya kubaki ndani ya timu hiyo.
Barcelona imekubaliana kuongeza dili la miaka miwli na nyota huyo ambaye aliibuka mfungaji bora kwa msimu wa 2020/21 akiwa ametupia jumla ya mabao 30 ndani ya La Liga.
Mkataba wake ndani ya Barcelona unameguka mwezi huu na mpaka anaenda mapumziko baada ya kupewa na Kocha Mkuu, Ronald Koeman alikuwa bado hajasaini dili jipya.
🙌🙌🙌✌✌
ReplyDelete