TIMU ya U 20 ya Mtibwa Sugar jana imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vijana.
Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa Azam Complex ambapo vijana wa Prisons walikubali kuokota wavuni bao moja mapema kabisa dakika ya pili lililopachikwa na Omary Marungu.
Bao hilo lilidumu mpaka dakika ya 90 ilipokamilika na kuwafanya Mtibwa Sugar wasepe na ushindi huo jumlajumla.
Pia katika mchezo mwingine uliochezwa jana ikiwa ni hatua ya nane bora mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex pia kati ya Kagera Sugar na Azam FC ulikusanya mabao matano yakiwa ni mengi kwa msimu huu katika hatua hii.
Ni baada ya dakika 90 kukamilika na ubao kusoma Kagera Sugar 2-3 Azam FC.
0 COMMENTS:
Post a Comment