NYOTA wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Israel Mwenda amesema kuwa aliambiwa apige pigo huru na Mohamed Hussein ambaye wanacheza naye.
Jana, Juni 13 kwenye Uwanja wa Mkapa, Stars iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Malawi ambapo watupiaji walikuwa ni John Bocco ambaye ni nahodha pamoja na Mwenda ambaye alipachika bao la pili kwa pigo huru akiwa nje ya 18.
Mwenda amesema:" Mohamed Hussein aliniambia nipige ile Free Kick( pigo huru) ndio maana nilipiga. Huwa nafanya mazoezi sana ya free kick ndio maana huwa nafunga mabao ya namna hiyo.
“Namshukuru Mungu na najiskia faraja kwa kucheza na kuiwakilisha nchi yangu, pia kuweza kufunga katika mchezo jambo hili litakaa katika kumbukumbu za maisha yangu yote.Mchezo huo ulikuwa ni wa kirafiki ambao upo kwenye kalenda ya Fifa ulihudhuriwa na mashabiki wengi ambao walijitokeza kuipa sapoti Stars.
0 COMMENTS:
Post a Comment