June 14, 2021


BERNARD Morrison kiungo mshambuliaji wa Simba amesema kuwa anachokifikiria akiwa uwanjani ni kuwapa furaha mashabiki wa timu hiyo jambo ambalo linamfanya azidi kujituma zaidi.

Nyota huyo ndani ya Simba amekuwa ni chaguo la kwanza la Didier Gomes kwa vijana wake ambao wataanzia benchi kuingia ndani ya uwanja kutokana na rekodi kumbeba.

Katika mechi alizoanzia benchi Morrison alikuwa akifanya vizuri ambapo miongoni mwa mechi alizofanya hivyo ilikuwa Uwanja wa Mkapa wakati ubao ukisoma Simba 1-1 Tanzania Prisons alitoa pasi kwa mshikaji wake Luis Miquissone.

Pia kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Majaliwa alipachika bao akiwa nje ya 18 kwa pasi ya Hassan Dilunga na kufanya ubao kusoma Namungo 1-3 Simba.

Nyota huyo amesema:"Ambacho huwa ninafikiria ni furaha kwa mashabiki wa timu pamoja na kuona kwamba kila kitu kinakwenda sawa tunapokuwa uwanjani jambo ambalo linafanya ninapambana kwa kushirkiana na wenzangu," .

Simba kwenye msimamo ipo nafasi ya kwanza imekusanya jumla ya pointi 67 baada ya kucheza mechi 27.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic