June 26, 2021


BAADA ya kutoka 
kifungoni, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela ameibuka na kutamka kuwa mapambano yanaendelea. 

Mwakalebela sasa yupo huru kuendelea kuitumikia klabu yake ya Yanga baada ya adhabu yake kutenguliwa na Kamati ya Rufaa ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

 

Kamati ya maadili ya TFF, imemuondoa kifungoni Mwakalebela, mara baada ya kiongozi huyo kukiri kosa lake na kuomba kuondolewa adhabu hiyo.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Mwakalebela alisema anajisikia furaha kurejea katika nafasi yake ya kuwatumikia Wanayanga.

 

Mwakalebela alisema kuwa kikubwa ataendelea na pale alipoishia katika nafasi yake ya uongozi katika klabu hiyo ambayo kesho inatarajiwa kufanya mkutano wake wa kihistoria kwenye Ukumbi wa DYCC, Changombe karibu ya Uwanja wa Mkapa, Dar.

 

“Binafsi nishukuru Kamati ya Rufani ya TFF kwa kutenda haki katika maamuzi yake ambayo jana (juzi), iliondoa adhabu ya kunifungia miaka mitano.

 

“Hivyo niwaambie Wangayanga nitaendelea na mapambano kama kawaida, nikiwa katika kifungo walinipa ushirikiano mzuri na kunifariji kwa kipindi chote, niwaahidi kuendelea kuwatumikia,” alisema Mwakalebela.

 

Kwa upande wa uongozi wa Yanga kwa kupitia Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa timu hiyo, Hassani Bumbuli alisema kuwa: “Kurejea kwa makamu mwenyekiti wetu tumepokea kwa furaha kubwa kama viongozi kwani kunaongeza nguvu kwenye ujenzi wa klabu.

 

“Alipokosekana kwenye uongozi kuna baadhi ya vitu vilikuwa haviendi sawa ikiwemo suala la mabadiliko ya klabu na kusababisha kupunguza kitu kikubwa, hivyo kurejea kwake kutaongeza nguvu.

6 COMMENTS:

  1. Utulie sasa uache kuropoka ropoka

    ReplyDelete
  2. Kweli kabisa maana manara haguswi hata akiwatukana VIP

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ushahidi muhimu sio maneno tu

      Delete
  3. Kutukana ni kosa wakitukana Yanga, wengine wanaambiwa wanafanya utani, ndio TFF ya sasa

    ReplyDelete
  4. Nyie manazi wa Utopolo ndio mnaowasababishia matatizo viongozi wenu kwa sababu ya mihemko isiyokuwa na tija

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic