IMEELEZWA kuwa hatma ya nyota watatu wa Simba ambao kandarasi zao zinakaribia kuisha msimu utakapokamilika zipo mikononi mwa Kocha Mkuu, Didier Gomes.
Wakati nyota hao watatu mikata yao ikitarajiwa kumeguka msimu huu wa 2020/21 utakapokamilika imeelezwa kuwa wamechuniwa na mabosi wao kwa kuwa hakuna ambaye amezungumza nao.
Ni Ally Salim kipa namba tatu wa Simba ambaye msimu huu hajacheza mchezo hata mmoja ndani ya ligi, Gadiel Michael beki na Ibrahim Ajibu kiungo mshambuliaji hawa pia wamekuwa hawana uhakika wa kuanza kikosi cha kwanza.
Taarifa zimeeleza kuwa mpaka sasa hakuna kati ya hao ambaye ameitwa na mabosi wa Simba ili kuzungumza nao kuhusu kuongeza mkataba.
"Wachezaji watatu bado hawajaitwa mpaka sasa kuzungumza na uongozi wa Simba kuhusu mikataba yao na ukizingatia kwamba bado ligi inaendelea hivyo bado kuna muda.
"Mwenye maamuzi ni kocha ambaye kupitia ripoti yake itaamua nani ambaye ataweza kubaki na ambaye ataondoka hivyo ni suala la kusubiri," ilieleza taarifa hiyo.
Hivi karibuni, Didier Gomes alisema kuwa anaamini katika uwezo wa wachezaji wake na wale ambao wanafanya vizuri atapenda kuendelea kubaki nao.
0 COMMENTS:
Post a Comment