June 15, 2021

 


KESHO Juni 16 inatarajiwa kuwekwa wazi juu ya wagombea ambao wamepenya hatua ya uchaguzi katika Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF).

Mchakato wa uchaguzi kwa sasa unaendelea ambapo Juni 12 ilikuwa ni mwisho wa kuchukua na kurejesha fomu kwa wagombea.

Jumla ya wagombea 6 walikamilisha zoezi hilo kwa upande wa nafasi ya Urais ikiwa ni pamoja na Oscar Oscar, Wallace Karia ambaye anatetea kiti chake, aLLY Mayay, Ally Saleh, Evans Mgeusa na Hawa Mniga.

Pia ni wajumbe 26 ambao wanawania nafasi hiyo katika kanda 6 tofauti ikiwa ni pamoja na Jimmy Mshindo, Saady Khimji, Lameck Nyambaya, Liston Katabazi, Hosseah Lugano, Elisony Mweladzi na Athuman Kambi kwa kanda namba 1 ya Dar na Pwani.

Wengine ni Khalid Mohamed, Zakayo Mjema na Thabity Kandoro kwa kanda ya Arusha ambayo ni namba mbili.


Kwa mujibu wa taarifa zinaeleza kuwa leo ni siku ya mwisho kwa kamati kukaa chini kupitia mchujo wa awali na kesho majina yatabandikwa kwenye ubao wa matangazo. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic