June 26, 2021


 SIMBA ikiwa imetwaa taji la Kombe la Shirikisho mara mbili inakwenda kukutana na Yanga iliyotwaa taji hilo mara moja katika mchezo wa fainali unaotarajiwa kuchezwa Kigoma.

Mchezo wa leo Juni 26 ambao ulikuwa ni wa nguvu kubwa na akili nyingi ulishuhudia Simba ikipachika bao la ushindi dk 89 kupitia kwa Luis Miquissone aliyetumia pasi ya Bernard Morrison.

Ni bao hilo liliibua utata kwa wachezaji wa Azam FC wakiongozwa na nahodha Agrey Morris ambao walionekana wakimzoga mwamuzi wa mchezo huo kwa kile walichokuwa wakionekana kulalamika Morrison kuanzisha mpira kwa haraka.

Licha ya wachezaji kulalamika na kuonyeshwa kadi za njano ikiwa ni kwa Bruce Kangwa bado mwamuzi aliweka mpira kati na ngoma ikakamilika Azam FC 0-1 Simba, Uwanja wa Majimaji.

Ushindi huo unaifanya Simba kuifuata hatua ya fainali Yanga ambayo jana ilishinda bao 1-0 dhidi ya Biashara United katika nusu fainali ya kwanza.

5 COMMENTS:

  1. Tunatetea makombe yetu yote tuliyonayo msimu huu, utopolo na wenzake wakatetee kombe lao mapinduzi

    ReplyDelete
  2. Hilo goli ni matokeo ya uziefu wa mechi kubwa. Azam walipashwa kumkinga morrison asipate kuanzisha mpira kabla hawajajipanga.

    ReplyDelete
  3. Goli la utata faulo inapigwa bila refa kuhesabu hatua, yaan unazi mtupu, Azam FC Mungu atawalipia siku ya fainal ya FA. Ni suala la muda tu

    ReplyDelete
  4. kufuatana na sheria timu inayohitaji muda ni ambayo imechezewa rafu! Simba pale hawakuhitaji muda...Kumbuka ni goli kama hilo Simba waliwafunga Nkana Red na kuwatoa CAF...kwani wale waamuzi walisemaje? ni sawa na mwamuzi wa leo. Tena ile faulo kama ingekuwa ni mwamuzi aliyechezesha mechi iliuopita ya Simba na Yanga na ni Tuisila ameangushwa palepale alipoangushwa Morrison..Unakumbuka pia Simba ilipokuwa nyuma kila wakianzisha faulo za dead ball anazuia hadi yeye ndiyo apulize filimbi...ilifika hatua wachezaji wa Simba walimzonga...Walichofanya Simba leo ni halali kwani sheria inaruhusu...Na ilikuwa faulo halali wachezaji wa Azam hawakupaswa kwenda kulalamikia faulo...walipaswa kushika mpira ili wakiwa tayari wampe morrison.Walimuacha

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wewe unajua sheria za mpira kweli kweli na pia una kumbu kumbu nzuri sana. Hongera zako mwanawane

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic