June 26, 2021


 UONGOZI wa Yanga umerejesha shukrani kwa mashabiki wake ambao walijitokeza kwa wingi jana Juni 25, Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya nusu fainali.

Mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Biashara United na mtupiaji akiwa ni Yacouba Songne.

Ushindi huo unafanya timu hiyo itinge hatua ya fainali ambapo sasa ni rasmi itakutana na Simba ambayo imecheza leo mbele ya Azam FC.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Kigoma na unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa watani hao wa jadi.

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa ni jambo la furaha kwa timu hiyo kutinga fainali hivyo mashabiki wanastahili pongezi.

4 COMMENTS:

  1. Wamerudishaje hiyo shukrani? Kwa ushindi?

    ReplyDelete
  2. Safi. Huo ndio uwanamichezo. Enzi za chuki tuziache nyuma. Sasa kazi

    ReplyDelete
  3. Kwakuwa kuwa keshafanikiwa makombe yote kama alivoahidi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic