June 18, 2021


 MTIBWA Sugar U 20 imewanyoosha Simba U 20 katika mchezo wa Ligi ya Vijana uliochezwa Uwanja wa Azam Complex katika hatua ya nusu fainali, Juni 17.

Ni Joseph mkele dk 14, Omary Marungu dk 54 kwa mkwaju wa penalti na bao jingine alipachika dakika ya 80 kwa upande wa Mtibwa Sugar.

Bao pekee la Simba U 20 lilipachikwa na Kassim Omary dk 68.Kupoteza kwa mchezo huo kunaifanya Simba U 20 kuikwepa Yanga katika mchezo wa fainali.

Pia mchezo mwingine wa nusu fainali uliowakutanisha Yanga v Azam FC, mshindi alipenya Yanga kwa penalti 6-5 baada ya dakika za awali ngoma kuwa 1-1.

Bao la Yanga lilifungwa na Abdulkarim Yunus dk 69 na lile la Azam FC lilifungwa na Ibrahim Issa dk 86.

Hivyo mchezo wa fainali ya Ligi ya Vijana U 20 inatarajiwa kuchezwa Juni 19 kati ya Yanga v Mtibwa huku Simba v Azam itacheza kumsaka mshindi wa tatu.

1 COMMENTS:

  1. Kwa haya maandishi mikia no Comment by into reality level hizi Simba mmekwama,hata kwa Wadada Ni hayo ya matokeo ya Mpira TZ

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic