June 17, 2021


UONGOZI wa Simba umeweka wazi kwamba upo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi Polisi Tanzania unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Ushirika, Moshi, Juni19.

Tayari kikosi cha Simba kipo Moshi ambapo kiliwasili jana, Juni 16 kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Mchezo wa kwanza walipokutana Uwanja wa Mkapa, ubao ulisoma Simba 2-0 Polisi Tanzania hivyo kisasi kwa Polisi itakuwa kushinda na Simba itakuwa na kazi ya kulinda rekodi zake.

Akizungumza na Saleh Jembe, Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mechi hiyo pamoja na zote ambazo zimebaki.

"Tupo tayari kwa ajili ya mechi zetu na kila mmoja anajua kwamba tunahitaji pointi tatu. Kikubwa ni kuona kwamba tunashinda kwani hilo ni jambo muhimu.

"Mashabiki watupe sapoti kwa ajili ya mchezo huo na tunatambua kwamba utakuwa ni mgumu kwa kuwa tunakutana na timu nzuri," amesema.

Kwenye msimamo wa ligi, Simba ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 67 baada ya kucheza 27, inakutana na Polisi Tanzania iliyo nafasi ya 7 na pointi 41. 

5 COMMENTS:

  1. Hivi Hawa Simba,Wana viporo Kwanini wanajipangia muda wa kucheza?

    ReplyDelete
  2. Mchezo unapigwa CCM Kirumba au Ushirika Moshi?Mwenye kuiweka hii sawa tafadhali

    ReplyDelete
  3. Mechi iko Mwanza mwandishi umekazana Moshi wewe vipi? Moshi kuna uwanja wa kuchezea simba kweli? Ule saizi yao yanga na ihefu

    ReplyDelete
  4. Anauliza hapo juu Simba ina viporo vipi inajipangia wenyewe michezo na jawabu ni kuwa Simba mwanamme na mfalme wa mpira ndio mana anajipangia mwenyewe na wadhaifu hawawezi kufanya hivo

    ReplyDelete
  5. Wanajipangia vipi?Mechi Polisi ndio wenyeji na wameihamisha kutoka Moshi uwanja wa Ushirika hadi Kirumba CCM Mwanza.
    Utopolo hata visivyowahusu wanalalamika.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic