June 17, 2021

 


NYOTA watatu wa kikosi cha Ruvu Shooting wanatarajia kuukosa mchezo wa leo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nassredine Nabi.

Ruvu Shooting inayonolewa na Kocha Mkuu, Charles Mkwasa inatarajia kukosa huduma ya nahodha wao Juma Nyosso pamoja na kipa wao namba moja Abdala Rashid ambao hawa wanatumikia adhabu ya kadi nyekundu waliyopata kwenye mchezo wao wa ligi dhidi ya Simba.

Pia kiungo wao fundi wa kuchezea mpira Abdurhaman Mussa atakosekana kwa kuwa ni majeruhi.

Kwa upande wa Yanga ni watatu ambao ni kiungo wao Balama Mapinduzi huyu bado hajawa fiti pamoja na Yassin Mustapha ambao walikuwa wanatibu majeraha huku Fiston Abdulazak akiwa hayupo kwenye mpango wa kocha.

Kwa mujibu wa Kocha wa makipa Razack Siwa alisema kuwa wachezaji wote wanaendelea vizuri hivyo itategemea na hali zao ili kuona nani ataanza leo.

4 COMMENTS:

  1. Na yule muangola aliyekimbia timu

    ReplyDelete
  2. Mechi haijasogezwa muda yanga wakimbie,

    ReplyDelete
  3. Ruvu ni wateja wa Yanga jumla jumla hakuna mpira hapo.

    ReplyDelete
  4. Wengine ni mapovu tupu, hebu pelekeni hela za mboga nyumbani

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic