RAHEEM Sterling amesisitiza kwamba uwezo wake kuonekana ni mbovu ndani ya Manchester City hauna uhusiano na kile ambacho anakifanya kwa sasa ndani ya timu ya taifa ya England baada ya kupachika bao moja la ushindi katika mchezo wa wa kwanza wa Euro 2020 mbele ya Croatia.
Sterling amewashangaza wengi kutokana na uwezo wake baada ya kumalizia pasi ya Kalvin Phillips dakika ya 57 mbele ya Dominik Livakovic ambaye alikuwa amekaa langoni.
Baada ya kusepa na pointi tatu hizo wakiwa katika kundi D kumemfanya Sterling awe na furaha kwa kufunga bao pekee la ushindi na kubainisha kwamba anafurahi kucheza na kuifungia timu yake ya taifa.
Nyota huyo amesema kuwa kuna mambo mengi ambayo yamemfanya ashindwe kufunga kwenye timu yake ya Manchester City lakini yeye anapenda kufunga kila anapopata nafasi.
"Kuna mambo mengi ambayo yanasababisha nishindwe kufunga kwenye timu yangu lakini kwa nilichofanya hapa na England ninafurahi sana na ni muhimu kwangu kuwa na furaha. Kwa nafasi ambayo nimepata na kufunga ni muhimu kwangu na furaha pia," .
0 COMMENTS:
Post a Comment