BAADA ya timu ya Taifa ya Netherlands kuichapa mabao 3-2 Ukraine katika michuano ya Euro 2020, mchambuzi wa masuala ya michezo, Roy Keane amesema kuwa tatizo la ulinzi litaimaliza mapema timu hiyo.
Katika mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Amsterdam Arena timu zote zilikuwa zikionyesha ufundi katika kucheza mpira pamoja na mbinu kali usiku wa kuamkia leo.
Ni Georginio Wijnaldum alianza kupachika bao la kuongoza dakika ya 52 kisha Wout Weghorst alipachika la pili dakika ya 58 na mabao hayo yaliwekwa usawa na Andriy Yarmolenko dk 75 na Roman Yaremchuk dk 79 kwa Ukraine.
Bao la ushindi lilipachikwa na Denzel Dumfries dakika ya 85 na kuwafanya Ukraine kupoteza pointi tatu mazima ndani ya kundi C katika mchezo wao wa kwanza.
Keane amesema:"Pongezi nyingi kwa Netherlands namna walivyoweza kuwa imara ila kwa mwendo ambao wameanza nao Ukraine wana kazi ya kufanya katika ulinzi," .
:d
ReplyDelete