KAMPUNI ya kutengeneza vifaa vya michezo UMBRO (South Africa) imeingia makubaliano na Clouds Media Group pamoja na SHADAKA Management kutengeneza vifaa vya michezo (jezi na mipira) kwa ajili ya michuano ya Ndondo Cup 2021.
Kwenye makubaliano hayo, Kampuni ya UMBRO itatengeneza jezi kwa ajili ya timu 32 zitakazocheza hatua ya makundi msimu huu pamoja na jezi kwa ajili ya waamuzi.
Kampuni ya UMBRO pia itatoa mipira yenye ubora uliothibitishwa na FIFA (International Match Standards) ambayo itatumika kwenye michuano ya Ndondo Cup kwa msimu huu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Ndondo Cup, Shaffih Dauda amesema kuwa mara zote wanaangalia ushirikiano na nembo kubwa.
“Kwenye malengo yetu ya kuwa mashindano bora ya mtaani Afrika, Ndondo Cup mara zote inaangalia kwenye kutengeneza ushirikiano na brand kubwa ndio maana tumeamua kushirikiana na Umbro”, amesema.
Naye Mkurugenzi wa Umbro South Africa, Byron Mulholland amesema:“Ndondo Cup ni sehemu sahihi kwa vijana kuonesha vipaji vyao vya soka Tanzania na mashindano hayo yanatoa mchango kwenye maendeleo ya soka la ndani la Afrika.
“Ushirikiano huu unaenda mbali zaidi ya Umbro kuingia kwenye soka la Tanzania, tunataka kufanyakazi na soka la ndani Afrika nzima. Tumefurahi kupata fursa hii na tunatarajia kuendelea kushirikiana zaidi na wengine ndani ya Tanzania," .
0 COMMENTS:
Post a Comment