June 4, 2021


 INASEMEKANA kuwa jina la kiungo mchezeshaji 
wa Simba, raia wa Kenya, Francis Kahata, limeingia kwenye rada za Azam FC katika usajili wa msimu ujao.

Hiyo ikiwa ni siku chache tangu tetesi zizagae Simba kuwepo katika mipango ya kuachana na kiungo huyo mwenye rasta baada ya mkataba wake kumalizika.

Kahata hivi sasa ni mchezaji huru anayeruhusiwa kufanya mazungumzo na klabu nyingine baada ya mkataba wake kumalizika tangu wiki iliyopita huku ikielezwa kurejea nyumbani kwao Kenya.

Taarifa ambazo imezipata Championi Ijumaa, jina la kiungo huyo linatajwa kuwepo kwenye orodha ya wachezaji wanaowaniwa na timu hiyo katika msimu ujao.



“Azam wamekuwa hawana kiungo mchezeshaji mwenye uwezo wa kuchezesha na kutuliza mashambulizi wakati timu inapozidiwa zaidi ya Sure Boy (Salum Aboubakary).

“Hivyo hivi sasa wapo katika mipango ya kumsajili Kahata kwa ajili ya kuiimarisha safu yao ya kiungo katika kuelekea msimu ujao.

“Na kingine wanachotaka kumsajili Kahata ni kwa ajili ya michuano ya kimataifa ambayo wana uhakika nayo watashiriki mwakani, hivyo kwa uzoefu wake ataisaidia timu hiyo,” kilisema chanzo hicho.


Alipotafutwa Mkuu wa Maudhui ya Simba, Ally

Shanty kuzungumzia hilo alisema hana taarifa

za Kahata kwani hayupo na timu hivi sasa tangu

timu ilipotolewa katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Kama unavyofahamu Kahata alisajiliwa kwa ajili ya michuano ya kimataifa na siyo Ligi Kuu Bara, hivyo hayupo na timu kwa hivi sasa,” alisema Shanty.

Kwa upande wa Ofisa Habari wa Azam, Thabiti

Zakaria alisema: “Masuala ya usajili yote yapo

chini ya kocha ambaye yeye ndiye anajua asajili

mchezaji gani, hivyo hilo suala halijafika mezani

kwangu na kama mchezaji akisajiliwa basi ni

lazima tutamtangaza, hivyo tusubiri.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic