June 15, 2021


 TATU kwa sasa zinasakwa kuweza kushuka Ligi Daraja la Kwanza baada ya moja kuweza kutangulia ambayo ni Mwadui FC kwa kuwa ni lazima timu nne zishuke.


Pia mbili zinaweza kubaki kwa kucheza playoff ikiwa zitashinda ambazo ni zile zitakazomaliza nafasi ya 13 na 14. Hivyo vita ya kushuka daraja na kubaki ndani ya ligi msimu huu sio mchezo mwepesi.


Championi Jumatano linakuletea namna timu ambazo hazina uhakika wa kubaki ndani ya ligi ikiwa zitashindwa kupata matokeo namna  zitakavyopambana kuweza kupata pointi tatu namna hii:-


 Ruvu Shooting


Ina  pointi 37 imebakiwa na mechi nne baada ya kucheza mechi 30 ipo nafasi ya 10. Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire ameliambia Championi Jumatano kuwa watapambana kushinda mechi zote ili wabaki ndani ya ligi.



Mechi zake zibaki:-Yanga, Juni 17, mchezo wa kwanza ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Yanga 2-1 Ruvu Shooting.Juni 24, Polisi Tanzania, Uwanja wa Mabatini, mchezo wa kwanza ngoma ilikuwa 0-0.


Julai 14, Namungo, Uwanja wa Mabatini, Uwanja wa Majaliwa, ubao ulisoma Namungo 2-1 Ruvu. Azam FC Julai 18,Mabatini,mchezo wa kwanza Azam FC 2-2 Ruvu Shooting.


 Mtibwa Sugar

Ipo nafasi ya 11 na pointi 34. Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru aliliambia Championi Jumatano kuwa wana mechi ngumu watampambana kupata matokeo ili wabaki ndani ya ligi.


 Mechi zake ni dhidi ya Mwadui, Juni 17, Uwanja wa Mwadui Complex, mchezo wa kwanza, Mwadui 0-1 Mtibwa Sugar. KMC, Juni 21, Uwanja wa Uhuru, mchezo wa kwanza Mtibwa Sugar 1-0 KMC.


 Dodoma Jiji, Julai 14, Uwanja wa Jamhuri,Dodoma, mchezo wa kwanza, Mtibwa Sugar 0-1 Dodoma Jiji.

JKT, Julai 18, Uwanja wa Samora, Iringa, mchezo wa kwanza JKT Tanzania 0-1 Mtibwa Sugar.


 Ihefu FC

Ipo nafasi ya 12 ina pointi 34. Zuber Katwila, Kocha Mkuu wa Ihefu aliliambia Championi Jumatatu kuwa amewaambia wachezaji wake wajiamini ili wapate matokeo mechi zilizobaki.


Mechi zake:-JKT,Juni 16, Uwanja wa Jamhuri,Dodoma, mchezo wa kwanza Ihefu 1-1 JKT Tanzania.

 Kagera, Juni 20, Uwanja wa Kaitaba mchezo wa kwanza, Ihefu 2-1 Kagera Sugar.

Yanga, Julai 14, Uwanja wa Mkapa, mchezo wa kwanza Ihefu 0-3 Yanga.

KMC, Julai 18, Uwanja wa Uhuru, mchezo wa kwanza Ihefu 1-0 KMC.


Kagera Sugar

Ina pointi 33 ipo nafasi ya 13, Francis Baraza, Kocha Mkuu wa Kagera Sugar alisema :”Mechi za mwisho kwetu ni fainali na tutashinda,”.


 Mechi zake:-Tanzania Prisons, Juni 16, Uwanja wa Kaitaba, mchezo wa kwanza, Tanzania Prisons 0-1 Kagera Sugar.

 Ihefu FC, Juni 20, Uwanja wa Kaitaba, walipokutana awali Ihefu 2-1 Kagera Sugar.


Polisi Tanzania, Julai 14, Uwanja wa Ushirika Moshi, awali matokeo ilikuwa Kagera Sugar 2-2 Polisi Tanzania.

 Coastal Union, Julai 18, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, Desemba 18, awali ilikuwa Kagera Sugar 3-1 Coastal Union.


Mbeya City

Ipo nafasi ya 14 ina pointi 33, mechi zake zilizobaki ni dhidi ya Coastal Union, Juni 18, Uwanja wa Sokoine, mchezo wa kwanza ilikuwa 0-0.


Juni 22, Simba v Mbeya City, mchezo wa awali Mbeya City 0-1 Simba. Gwambina, Julai 14, Uwanja wa Sokoine, mchezo wa awali, ubao ulisoma 1-1.


 Biashara United, Julai 18,Uwanja wa Sokoine. walipokutana Uwanja wa Karume, Mara, Desemba 18 ubao ulisoma Biashara United 3-0 Mbeya City.


 

 JKT Tanzania

Ipo nafasi ya 15 ina pointi 33. Mohamed Abdalah, Kocha Mkuu wa JKT Tanzania ameliambia Championi Jumatano kuwa wanatambua wapo sehemu mbaya hivyo lazima washinde mechi zao.


Mechi zao ni:-Ihefu FC, Juni 16, Uwanja wa Jamhuri,Dodoma. Mchezo wa awali Ihefu 1-1 JKT Tanzania.

 


Biashara United, Juni 20, Uwanja wa Karume, mchezo wa kwanza JKT 2-0 Biashara United.

 KMC, Julai 14, Uwanja wa Uhuru, Desemba 23, Uwanja wa Jamhuri, mchezo wa kwanza JKT Tanzania 2-0 KMC.

 Mtibwa Sugar, Julai 18, Uwanja wa Samora, Iringa,mchezo wa awali ilikuwa JKT Tanzania 0-1 Mtibwa Sugar.



 Coastal Union

Ipo nafasi ya 16 ina pointi 33, Juma Mgunda, Kocha Mkuu wa Coastal Union aliliambia Championi Jumatano kuwa kazi inaendelea.


Mechi zao:-Mbeya City, Juni 18, Uwanja wa Sokoine, mchezo wa kwanza ilikuwa 0-0

 Tanzania Prisons, Juni 22, Uwanja wa Nelson Mandela , mchezo wa kwanza ilikuwa 0-0.

Simba, Julai 11, Uwanja wa Mkapa , mchezo wa awali Coastal Union 0-7 Simba. Mwadui, Julai 14,Uwanja wa Mkwakwani, mchezo wa awali ilikuwa 0-0.

 Kagera Sugar, Julai 18, Uwanja wa Mkwakwani, mchezo wa awali, Kagera Sugar 3-1 Coastal Union.


 Gwambina

 Ipo nafasi ya 17 na pointi zake ni 31, mechi zake ni dhidi ya Azam FC, Juni 18, mchezo wa awali ilikuwa 0-0.


 Dodoma Jiji, Uwanja wa Gwambina Complex, Juni 23, mchezo wa awali ilikuwa Dodoma Jiji 1-0 Gwambina.


  Mbeya City, Uwanja wa Sokoine, Julai 14, mchezo wa kwanza ilikuwa 1-1.Julai 18, Tanzania Prisons, Uwanja wa Nelson Mandela,  mchezo wa awali ilikuwa 1-1.


 Mwadui FC

Tayari imeshashuka daraja ipo nafasi ya 18 na pointi 19. Mechi zake ni dhidi ya:- Mtibwa Sugar, Juni 17, Uwanja wa Mwadui Complex. Mchezo wa awali Mtibwa Sugar 1-0 Mwadui.


Yanga, Juni 20, Uwanja wa Mkapa, mchezo wa kwanza, Mwadui 0-5 Yanga.



Coastal Union, Julai 14, Mkwakwani, mchezo wa awali ilikuwa 0-0.Polisi Tanzania, Uwanja wa Ushirika Moshi, Julai 18, mchezo wa awali ulisoma 1-1.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic