June 14, 2021


 UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kwamba mechi zao tano ambazo zimebaki sawa na dakika 450 watapambana kushinda ili kupata pointi tatu zitakazowapa jumla ya pointi 15.

Mechi zao ambazo zimebaki kwa sasa baada ya kucheza mechi 29 ni Juni 17  dhidi ya Ruvu Shooting, Juni 20 ni dhidi ya Mwadui, Julai 3 dhidi ya Simba, Julai 14 dhidi ya Ihefu na kigongo chao cha mwisho ni Julai 18 dhidi ya Dodoma Jiji.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli alisema kuwa wanahitaji pointi tatu katika kila mechi kwa kuwa wanajua umuhimu wa pointi hizo na nia yao ni kufikia malengo yao ya kutwaa ubingwa.

“Hatujakata tamaa kuhusu ubingwa kwani tuna mechi tano mkononi, katika hizo mechi tano tumepanga kushinda zote kisha baada ya ligi kukamilika hapo tutajua kwamba tumevuna nini na tunastahili kupata nini.

“Hao wanaoongoza ligi ikumbukwe kwamba wana viporo, sasa wakimaliza kucheza hizo mechi kisha tukiwa nao tumecheza mechi sawa itafahamika tu mwisho wa ligi,” alisema Bumbuli.

Vinara wa ligi ni Simba wana pointi 67 baada ya kucheza mechi 27 na Yanga wamecheza mechi 29 wana pointi 61.

3 COMMENTS:

  1. Wanaamini watashinda mechu zao tano na kujikusanyia poit 15 na huku na huku mnyama ikipoteza mechi zao zote zilizobaki na hivi ndivo akili zao hafifu zinavofanya kazi

    ReplyDelete
  2. Kwenye hzo 5 watashinda 3, sare 1 na iliyobaki wasipokimbia basi wanapasuka nyingi .... Kama mnabisha subirini muone

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic